Mambo Yote Mapya

OneVoice27 ni mpango unaolenga kuwaunganisha waumini wote duniani kuhubiri ujumbe wa Yesu Kristo kwa sauti moja, kupitia njia zote za mawasiliano na ushuhuda, kuelekea mwaka 2027 ambao utakua kumbukumbu ya miaka takribani 2,000 tangu ubatizo wa Yesu na kuanza kwa huduma yake kuihubiri injili na ukombozi wa wanadamu.

Wito huu ambao umezinduliwa rasmi tar. 05/09/2026 na kubeba neno kuu MAMBO YOTE MAPYA (Tumaini Linaanzia Hapa) unamhitaji kila muumini kushiriki na kuushirikisha ulimwengu upendo wa Yesu Kristo kupitia njia za kidigitali. Kila simu, kila tablet, kila iPad, kila computer na kila mtandano wa kijamii neno la Bwana liende kwa kila mwanadamu.